Baada ya kuwa naandika mara kadhaa kwenye mitandao ya kijamii na Mungu kunifumbua macho nione hitajio la kuwapo kwa habari za Kikristo katika mwanga na tafsiri pana ya habari, hii ni hatua ya kwanza kuelekea kutimiza jambo hilo ambalo naona kama ni wito wangu kuutekeleza.
Kwa hiyo nitoe tafsiri ya mambo kadhaa ya msingi, kwanza jina la Blog. Sauti ya mlinzi ni jina ambalo limekuja moyoni mwangu kwa sababu ya kutambua kwamba vyombo vingi vya habari za Kikristo nchini Tanzania vimekuwa vikitoa habari hizo kwa msingi wa kufikisha tu ujumbe na mafundisho, lakini ni vichache na kwa sehemu ndogo vinajaribu kuangalia mambo na kuyafanyia uchambuzi kwa misingi ya unabii wa neno la Mungu na hivyo kuwaandaa watu juu ya ni nini kinaweza kutokea mbeleni na jinsi wanavyoweza kufanya.
Ndipo katika kulisoma neno takatifu la Mungu katika kitabu cha nabii Ezekiel 33:2 nikakutana na maneno yafuatayo (tafsiri ya mwandishi kutoka KJV) "Mwanadamu, sema na wana wa watu wako kusema, Ikiwa nitautuma upanga juu ya nchi, ikiwa watu watamtwaa mtu mmoja wa kwao na kumweka kuwa mlinzi wao.....akiona upanga unakuja apige tarumbeta na kuwaonya watu...." na ndipo itakuwa kazi ya Blog hii kupiga tarumbeta. Kutafsiri matukio katika ulimwengu wa kichumi katika mwanga wa neno la Mungu.
Karibu, usiche kutembelea mtandao huu kuanzia tarehe 15 June 2012. Hapa tutatembea duniani kwenye ulimwengu wa Uchumi na Biashara, Siasa na Sayansi na kuyatazama matukio ya ulimwengu kutokea kwenye mwanga wa Biblia na unabii uliomo ndani yake.
Nakutakia usomaji mwema. Unaweza kuandikisha e-mail yako ili utumie ujumbe moja kwa moja kila tunapoweka habari mpya, lakini ni kusudi letu kwamba kila siku kuanzi jumatatu hadi Jumamosi, tukuletee habari na matukio kutoka ulimwengu wa Kikrsto.

No comments:
Post a Comment